Yanga wako mbali zaidi ya Simba – Edo Kumwembe
Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Edo Kumwembe amehoji iwapo Klabu ya Yanga wanaona mbali zaidi kwenye masuala ya usajili kuliko wapinzani wao Klabu ya Simba.
Edo amesema hayo baada ya Simba kuachana na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wake, Said Ntibanzokiza maarufu kama Saido ambaye pia amewahi kuitumikia Yanga kabla ya kuitumikia Geita Gold kisha Simba.
“Safari hii Simba wamedai kwamba Saido amechoka kwa nini hawakuliona hili wakati Yanga walipokuwa wanamchukua na wao ndio walikuwa wanasema hili? Kwanini hawakuliona hili wakati baadhi ya watu wa Yanga walipolisema hili wakati wanaachana naye?
“Labda kwa kudharau kile ambacho Yanga walikuwa wanakisema kisha wao wakambeba huenda ndio ilikuwa ni miongoni mwa anguko la Simba na kupanda kwa Yanga katika miaka ya karibuni? kwamba kwa miaka ya karibuni Yanga huwa wanaona mbali kuliko wao??" -- alisema Edo Kumwembe.
Yanga wako mbali zaidi ya Simba – Edo Kumwembe
Reviewed by Zero Degree
on
6/27/2024 06:57:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
6/27/2024 06:57:00 AM
Rating:
