Firmino atimiza ndoto yake ya kuwa mchungaji
Nyota wa zamani wa Liverpoon na Brazil, Roberto Firmino kwa kushirikiana na mkewe, wameanzisha kanisa huko Maceio, Brazil ambalo yeye atakuwa miongoni mwa wachungaji.
Kufunguliwa kwa kanisa hilo ni kutimia kuwa ndoto ya muda mrefu kwa Firmino kufanya huduma ya uchungaji yeye pamoja na mkewe Larissa Pereira.
Eneo la Maceio alikoanzisha kanisa hilo ndio mahali ambako mshambuliaji huyo wa Al Ahli ya Saudi Arabia alizaliwa miaka 32 iliyopita.
Firmino anakumbukwa kwa mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya Liverpool katika kipindi cha miaka nane aliyoitumikia kabla ya kutimkia Saudi Arabia.
Akiwa na Liverpoo alifunga mabao 111 katika mechi 362 alizoitumikia huku akipiga pasi 75 za mwisho.
Mabao ya mshambuliaji huyo yalichangia kwa kiasi kikubwa kuiwezesha Liverpool kutwaa mataji ya Klabu Bingwa ya Dunia, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Calabao na FA.
Akiwa na Al Ahli, Firmino msimu uliomalizika alifunga mabao tisa na kupiga pasi za mwisho saba katika mechi 34.
Al Ahli ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia huku Al Hilal ikitwaa ubingwa.
Firmino atimiza ndoto yake ya kuwa mchungaji
Reviewed by Zero Degree
on
7/09/2024 06:04:00 AM
Rating: