HESLB yatangaza fursa kwa wahitimu wa shahada
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetangaza fursa ya mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) kwa wanafunzi na wahitimu wa shahada.
Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa X, HESLB imetangaza kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa kushirikiana na taasisi ya Adanian Labs. HESLB ilieleza kuwa mpango huo ni sehemu ya jitihada zake za kuwajengea uwezo wa kuajirika wahitimu wa shahada mbalimbali ambao pia ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na serikali kupitia bodi hiyo ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa na hivyo kuwa na uwezo wa kurejesha.
Mpango huu uanwalenga wahitimu wa shahada zenye mchepuo wa teknolojia ya habari na mawasiliano na sayansi ya kompyuta. “Aidha, wanafunzi wa kozi hizi waliopo katika mwaka wa mwisho wa masomo nao wanaweza kuomba,” ilieleza HESLB.
Pia wamefafanua kuwa watakaochaguliwa mafunzo yataendeshwa bure kwa miezi minne kwa njia ya mtandao kuanzia Agosti 5, mwaka huu. HESLB ilieleza kuwa wakati wa mafunzo kila mwanafunzi atapaswa kuwa na kompyuta na intaneti.
Pia wamefafanua kuwa watakaochaguliwa mafunzo yataendeshwa bure kwa miezi minne kwa njia ya mtandao kuanzia Agosti 5, mwaka huu. HESLB ilieleza kuwa wakati wa mafunzo kila mwanafunzi atapaswa kuwa na kompyuta na intaneti.
HESLB yatangaza fursa kwa wahitimu wa shahada
Reviewed by Zero Degree
on
7/25/2024 12:31:00 PM
Rating: