Maofisa ardhi wawili matatani kwa rushwa jijini Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amemwagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa kuwakamata maofisa wawili wa Idara ya Ardhi wa Manispaa ya Ilemela kwa tuhuma za kuomba rushwa.
Mtanda alitoa agizo hilo juzi katika Mtaa wa Igoma wakati wa mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi baada ya kuibuka madai ya maofisa hao kuomba rushwa wanapotoa huduma za upimaji viwanja kwa wananchi.
Mwananchi, Matiko Migire, akiwasilisha kero yake katika mkutano huo alidai kuwa maofisa hao walimwomba rushwa ya Shilingi milioni 2.43 kwa ajili ya kumpimia viwanja namba 311, 312 na 313 Block ‘A’ Pasiansi.

Magire alitoa madai hayo huku akiwa na viambatanisho vya ushahidi wa mawasiliano yake na maofisa hao kwa njia ya mtandao wa WhatsApp kuthibitisha kuombwa kulipa fedha kwa namba ya malipo ya serikali ya 'contral number' na kingine mkononi kinyume cha sheria.
Matiko aliendelea kudai kuwa mwaka 2019, halmashauri hiyo iliomba hati za viwanja hivyo na kuzifuta, kisha kuahidi kufanya upimaji mwingine na wamiliki wake, Joseph Mashiku, Hezeline Chawachi na Desderius Ntobi kuwapa namba ya kulipia gharama ya Shilingi 500,000.
Alidai idara hiyo haijawahi kutekeleza ahadi ya kwenye viwanja hivyo na badala yake wamekuwa wakimtafuta kwa simu mmoja wa maofisa hao na kumtaka atume kiasi hicho cha Sh.milioni 2.43 ikiwa fedha halali anayotakiwa kulipia ni Shilingi 500,000 tu.

Akijibu madai hayo, Mtanda alisema kitendo hicho si cha kiungwana na kinawanyima haki wananchi, wakati TAKUKURU wanachunguza, idara ya ardhi ilipewa siku saba kukamilisha upimaji viwanja hivyo.
Akizungumzia kero ya maji kwa baadhi ya mitaa ya Nyamagana, Mtanda alisema kupitia mkopo wa Sh. bilioni 400 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) itasambaza huduma hiyo umbali wa zaidi ya kilomita 700 kutoka chanzo cha Butimba hadi kwenye maeneo hayo.
Akizungumzia kero ya maji kwa baadhi ya mitaa ya Nyamagana, Mtanda alisema kupitia mkopo wa Sh. bilioni 400 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) itasambaza huduma hiyo umbali wa zaidi ya kilomita 700 kutoka chanzo cha Butimba hadi kwenye maeneo hayo.
Maofisa ardhi wawili matatani kwa rushwa jijini Mwanza
Reviewed by Zero Degree
on
7/18/2024 08:40:00 AM
Rating: