Loading...

Ngao ya Jamii: Yanga vs Simba, Azam Vs Coastal Agosti 8


Nusu fainali za michuano ya Ngao ya Jamii ikiwa ni ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu mpya 2024/2025 zitapigwa Agosti 8 Dar es Salaam na Zanzibar.

Yanga na Simba zitakutana katika nusu ya pili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam wakati Azam itavaana na Coastal Union katika nusu ya kwanza kwenye uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu utatangulia Agosti 11 kabla ya fainali kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, michuano ya Ngao ya Jamii itazikutanisha timu nne, bingwa wa ligi dhidi ya mshindi wa tatu na mshindi wa pili dhidi ya mshindi wa nne.

Bingwa mtetezi wa Ngao ya Jamii ni Simba iliyotwaa ubingwa katika fainali iliyopigwa Agosti 13, 2023.

Ligi Kuu Tanzania Bara imepangwa kuanza Agosti 16.

Yanga ndio bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimamo wa 2023/2024 iliyoshrikisha timu 16.

Timu zitakazoshiriki Ligi Kuu msimu wa 2024/2025 ni Yanga, Simba, Azam, Coastal Union, Dodoma Jiji, Singida Black Stars, JKT Tanzania, Kagera Sugar, KenGold, KMC, Mashujaa, Namungo, Pamba, Singida Fountain Gate, Tabora United na Tanzania Prisons.
Ngao ya Jamii: Yanga vs Simba, Azam Vs Coastal Agosti 8 Ngao ya Jamii: Yanga vs Simba, Azam Vs Coastal Agosti 8 Reviewed by Zero Degree on 7/19/2024 06:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.