Loading...

Nyimbo zangu ni kali sana, na sijawahi kufanya kazi mbaya - Inspekta


Inspekta Haroun, 'Babu' aliyewahi kutamba na ngoma zilizompa heshima kubwa kwa mashabiki ndani na nje ya Tanzania kama ‘Mtoto wa Geti Kali’, ‘Nje Ndani’ na ‘Asali wa Moyo’ aliliambia Mwanaspoti, kushindwa kuwekeza vyema katika muziki kwa sasa ndiko kunakomfelisha.

MKongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Haroun Rashid Kahena ‘Inspekta Haroun’ a.k.a Babu ni kama amejishtukia baada ya kusema amegundua kitu kinachomkwamisha kwa sasa kufanya vizuri katika fani hiyo, tofauti na ilivyokuwa zamani alipotamba na kundi na Gangwe Mobb akishirikiana na Luteni Karama.

“Nilichogundua ni kwamba kinanikwamisha kwa sasa ni uwekezaji tu. Kwa sababu nyimbo zangu ni kali sana na sijawahi kufanya kazi mbaya katika maisha yangu ya muziki, ila nakwamia hapo tu,” alisema Inspekta na kuongeza;

“Kama ningepata menejimenti nzuri ya kusimamia muziki wangu na kuwekeza ningerudi vizuri katika gemu kama zamani. Hata hivyo, siwezi kukata tamaa, napambana.”

Chanzo: Mwanaspoti
Nyimbo zangu ni kali sana, na sijawahi kufanya kazi mbaya - Inspekta Nyimbo zangu ni kali sana, na sijawahi kufanya kazi mbaya - Inspekta Reviewed by Zero Degree on 7/07/2024 12:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.