Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Julai, 2024
Barcelona wamekubali makubaliano ya awali kwa ajili ya mshambuliaji wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 21. (Sport)
Paris St-Germain iko tayari kushindana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa kimataifa wa Ureno Joao Neves, 19. (Le10Sport)
Manchester United wana nia ya kukamilisha usajili wa beki wa Bayern Munich Mholanzi Matthijs de Ligt, 24, haraka iwezekanavyo baada ya Euro 2024. (Bild)
Arsenal wamekubali ofa ya mkopo kutoka kwa Lazio kwa beki wao wa pembeni wa Ureno Nuno Tavares, 24 na kulazimika kumuuza kati ya £6m na £7m. (Mirror)
Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid huenda anakoelekea kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Juventus kumalizika mwezi uliopita. (Calciomercato)
Klabu ya Marseille wanavutiwa na mshambuliaji wa Arsenal na Uingereza Eddie Nketiah, mwenye umri wa miaka 25. (Footmercato)
Monaco imekataa dau la euro 30m (£25.5m) kutoka kwa Nottingham Forest kwa ajili ya kiungo wa kati wa Ufaransa Youssouf Fofana, 25, ambaye amekubali makubaliano na AC Milan. (Fabrizio Romano)
Bayern Munich wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Xavi Simons, 21, kutoka Paris St-Germain.
Beki wa kati wa Uingereza Jacob Greaves, 23, amekamilisha matibabu yake ya kuhamia Ipswich Town kabla ya kuondoka kutoka Hull City.
Chelsea hawana nia ya kuanzisha kipengele cha kumnunua mshambuliaji wa Uhispania Dani Olmo mwenye umri wa miaka 26 katika klabu ya RB Leipzig kwa pauni milioni 50. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 29, atakamilisha uhamisho wake kutoka Fulham hadi Bayern Munich katika muda wa saa 24 zijazo. (Sky Germany)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Julai, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
7/11/2024 08:35:00 AM
Rating: