Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 4 Julai, 2024
Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Nottingham Forest wa Uswidi Anthony Elanga, 22. (Teamtalk)
Borussia Dortmund itamnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, mwenye umri wa miaka 28, ikiwa watashindwa katika majaribio yao ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross, 33, kutoka Brighton . (Sky Sports Ujerumani)
Arsenal wameipiku Juventus katika harakati za kumsaka beki wa Bologna Riccardo Calafiori, 22, ambaye aliisaidia pakubwa Italia kwenye Euro 2024. (Telegraph)
Matthijs de Ligt ana nia ya kuhamia Manchester United , huku Bayern Munich wakithamini beki huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24 kwa euro 50m (£42.4m). (Sky Sports)
Paris St-Germain wameulizia kuhusu mshambuliaji wa Leeds United na Uholanzi Crysencio Summerville, 22. (De Telegraaf)
Manchester City wanajiandaa kumsajili winga wa Brazil Savio mwenye umri wa miaka 20 kutoka Troyes.
Klabu ya Brighton wanavutiwa na kiungo wa kati wa Feyenoord na Uholanzi Mats Wieffer, 24 na beki wa pembeni wa Rayo Vallecano wa Romania Andrei Ratiu, 26. (Athletic)
Manchester United wamefanya mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Bologna Joshua Zirzkee, ingawa AC Milan tayari wamekubaliana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, mwenye umri wa miaka 23 (Calciomercato).
Chelsea wamekubali ada ya £14m na Boca Juniors kwa ajili ya beki wa Argentina mwenye Aaron Anselmino, 19. (Football London)
Ofa ya West Ham ya euro 35m (£26.9m) imekataliwa na Nice kwa ajili ya mlinzi wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24.
West Ham have had a 35m euro (£26.9m) bid rejected by Nice for France defender Jean-Clair Todibo, 24. (L'Equipe)
Borussia Dortmund itamnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, mwenye umri wa miaka 28, ikiwa watashindwa katika majaribio yao ya kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross, 33, kutoka Brighton . (Sky Sports Ujerumani)
Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya Harry Maguire msimu huu wa joto, huku vilabu vya Italia vikiwa vinamtaka nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza, 31. (Talksport)
Burnley wanatazamiwa kumteua meneja wa zamani wa Fulham Scott Parker kama meneja mpya wa klabu hiyo.
Beki wa Swansea Nathan Wood atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu huko Southampton baada ya vilabu hivyo kukubaliana ada ya pauni milioni 5 kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza wa kikosi cha chini ya umri wa miaka 21, (Football Insider)
Wolves inamfuatilia kiungo wa Juventus Arthur Melo kabla ya uwezekano wa kumnunua Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27.
Kiungo wa kati wa Aston Villa Philippe Coutinho anatarajiwa kuondoka Villa wiki hii, huku Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 32 akitamani kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Vasco da Gama. (Birmingham Live)
Manchester United haijafutilia mbali uwezekano wa kumruhusu mshambuliaji Mwingereza Marcus Rashford, 26 kuondoka msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)
West Ham wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa na chini ya miezi 12 kwenye mkataba wake wa sasa. (Metro)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 4 Julai, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
7/03/2024 10:37:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
7/03/2024 10:37:00 AM
Rating:

