Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Julai, 2024

Joshua Zirkzee, 23

Manchester United wanatarajiwa kufikia kipengele cha kutolewa kwa Joshua Zirkzee cha pauni milioni 34 ili kumsajili fowadi huyo wa Uholanzi, 23, kutoka Bologna. (Mail)

Arsenal na Manchester United wako tayari kushindania kumsaini beki wa Uingereza Marc Guehi, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akitarajiwa kukataa ofa ya kandarasi mpya ya Crystal Palace. (Sun)

United inajadili iwapo itaanzisha kifungu hicho cha kutolewa au kujadili ada ya juu ambayo itaruhusu malipo kwa awamu.

Arsenal wanatarajia kukamilisha usajili wa Riccardo Calafiori wiki hii baada ya kufanya mazungumzo zaidi na Bologna kuhusu beki huyo wa Italia, 22. (Guardian)

Rais wa Barcelona Joan Laporta anasema klabu hiyo iko katika nafasi ya kumudu usajili wa winga wa Uhispania Nico Williams, mwenye umri wa miaka 21, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha £49m katika mkataba wake na Athletic Bilbao. (Catalunya Radio)

Ipswich wana uhakika wa kuwasaini wachezaji wawili wa Uingereza na Hull City - winga Jaden Philogene, 22, na mlinzi Jacob Greaves, 23, kwa takriban £35m. (Sportsport)

Everton wana imani kuwa wameishinda Crystal Palace katika kumsajili Philogene baada ya kufikia makubaliano na Hull. (TeamTalks)

Jacob Ramsey, 23

Tottenham wanatafuta dili la mchezaji pamoja na pesa kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa Muingereza Jacob Ramsey, 23, huku kiungo wa kati wa Argentina Giovani lo Celso, 28, akielekea Aston Villa. (Sky Sports)

Klabu ya Ubelgiji Beerschot inatazamiwa kuwasajili kiungo wa kati wa Hibernian raia wa Scotland Ewan Henderson, 24, na winga Mwingereza D'Margio Wright-Phillips, 22, ambaye ameondoka tu Stoke. (Nieuwsblad)

Stuttgart inapanga kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Brighton na Ujerumani Deniz Undav, 27. (Bild)

Nahodha wa zamani wa Wolves Danny Batth, mwenye umri wa miaka 33, amerejea klabuni hapo na kufanya mazoezi na vijana wa chini ya miaka 21 baada ya Beki huyo wa Uingereza Kuondoka Norwich. (Express & Star)

Tottenham Hotspur wana uhakika wa kumbakiza winga Mwingereza Mikey Moore, 16, licha ya Paris St-Germain na Real Madrid kumtaka. (HITC)

Luton ni miongoni mwa klabu zinazovutiwa na kiungo wa kati wa Mechelen Ngal'ayel Mukau, 19, ambaye anastahili kuichezea Ubelgiji au DR Congo. (HLN)

Chelsea wamefikia makubaliano na Atlanta United kumsajili beki wa kushoto wa Marekani Caleb Wiley, 19, kwa £8.5m - lakini wanatarajiwa kumtoa kwa mkopo kwa Strasbourg. (Sport)

Klabu ya Leeds United wanatarajiwa kuwauza winga wa Uholanzi Crysencio Summerville, 22, fowadi wa Ufaransa Georginio Rutter, 22, na mshambuliaji wa Italia Wilfried Gnonto, 20, msimu huu. (Football Insider)

Joshua Kimmich, 29

Bayern Munich inahitaji kuuza wachezaji kabla ya kusajili mtu yeyote - huku winga wa Ufaransa Kingsley Coman, 28, mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, viungo wa Ujerumani Leon Goretzka, 29, Joshua Kimmich, 29, na Serge Gnabry, 28, na Mlinzi wa wa kushoto wa Canada Alphonso Davies, 23, miongoni mwa wanaotaka kuondoka. (Kicker)

Beki wa Nice na Ufaransa Jean-Clair Todibo, 24, anataka kujiunga na Juventus baada ya uhamisho wake kwenda Manchester United kushindikana. (Gazeti)

Sevilla wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 29, kutoka Atletico Madrid. (SER).
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Julai, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 9 Julai, 2024 Reviewed by Zero Degree on 7/09/2024 08:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.