Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Julai, 2024


Manchester United wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 25, msimu huu wa joto. (HITC)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, anakaribia kusaini Manchester United baada ya kuondoka Juventus mwishoni mwa kandarasi yake. (Goal)

Arsenal wanajiandaa kumsajili mlinda mlango wa Uingereza Tommy Setford, mwenye umri wa miaka 18, kutoka Ajax kabla ya ziara yao ya Marekani. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Denmark Jesper Lindstrom, 24, yuko tayari kwa mkopo wa msimu mzima kwa Everton kutoka Napoli. (CalcioMercato)

Brighton wamefanya mazungumzo na Inter Miami kuhusu mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Paraguay, Diego Gomez, mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)

Everton watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips, 28.


Manchester United wameweka bei ya pauni milioni 30 kwa kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay, 27.

Aston Villa wanajiandaa kumuuza mlinzi wa Ufaransa Lucas Digne, 31.

Birmingham City wameelekeza macho yao kwa kiungo wa Fulham na Wales Luke Harris, mwenye umri wa miaka 19. (Football Insider)

West Ham wana makubaliano ya mdomo kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 33, kutoka Al Ittihad.

Arsenal wanaongeza juhudi zao za kumsajili beki wa Italia Riccardo Calafiori, 22, kutoka Bologna. (The Athletic)

Chelsea wanajiandaa kumpeleka kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 20, kwa mkopo Strasbourg tena baada ya kumalizika kwa ziara yao ya Marekani.


Kiungo wa kati wa Uruguay Manuel Ugarte, mwenye umri wa miaka 23, amekubali masharti ya binafsi na klabu ya Manchester United, ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na Paris St-Germain. (Fabrizio Romano)

Lille wanatafuta kumsajili mlinzi wa West Ham Morocco Nayef Aguerd, 28, kama mbadala wa beki Mfaransa Leny Yoro, 18, ambaye amesajiliwa na Manchester United. (L'Equipe)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Julai, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Julai, 2024 Reviewed by Zero Degree on 7/21/2024 09:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.