Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Julai, 2024


Real Madrid wanavutiwa na beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold, Aston Villa wanataka pauni milioni 60 kutoka kwa Al-Ittihad kumuuza Moussa Diaby, Marseille wakubali dili la kumnunua Mason Greenwood wa Manchester United.

Real Madrid wana hamu ya kumsajili beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 25, ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Liverpool. (Talksport)

Manchester United hawana nia ya kumnunua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate endapo wataamua kumfuta na Erik ten Hag. Badala yake, mkufunzi wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel anaonekana kupendelewa zaidi. (Mail)

Manchester United wanajadiliana kuhusu masuala ya kibinafsi na wawakilishi wa mlinzi wa Ufaransa Leny Yoro baada ya kupokea ofa ya pauni milioni 52 iliyokubaliwa na Lille kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake. Yoro pia ananyatiwa na Real Madrid.

Newcastle United wamesema watapambana kumbakisha mkufunzi wao Eddie Howe baada ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 kuhusishwa na tetesi za kuchukua nafasi ya Gareth Southgate aliyejiuzulu kama kocha wa Uingereza. (Guardian)

Aston Villa wanataka pauni milioni 60 kutoka kwa Al-Ittihad ikiwa klabu hiyo ya Ligi ya Saudi Pro inataka kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Diaby, 25. (Sportsport)

Marseille wamefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood, mwenye umri wa miaka 22. (The Athletic)

Aston Villa inajiandaa kumenyana na Chelsea na Barcelona kumsajili winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, 22 ambaye aliichezea Uhispania katika michuano ya Euro 2024. (Teamtalk)

Al-Nassr wamekamilisha mazungumzo ya kumsajili mlinda mlango wa Manchester City Ederson, 30, baada ya ofa yao ya euro 30m kukataliwa. Klabu hii ya Saudia sasa inajaribu kumsajili mchezaji mwenzake wa Brazil Bento, mwenye umri wa miaka 25, anayechezea Athletico Paranaense. (Fabrizio Romano)

Arsenal wanatarajia kupokea ofa zaidi kwa kiungo Emile Smith Rowe, mwenye umri wa miaka 23, baada ya kukataa ombi la Fulham la kumsajili Muingereza huyo, huku Crystal Palace pia wakimtaka. (Evening Standard)


Cole Palmer amejaribu kumshawishi mchezaji mwenzake wa England na mshambuliaji wa Aston Villa Ollie Watkins, 28, kujiunga na Chelsea msimu huu wa joto. (Football Insider)

Leicester City wamewasilisha ofa ya pauni milioni 21m na na nyongeza ya oauni milioni nne kwa ajili ya kiungo mshambuliaji wa Argentina Matias Soule, mwenye umri wa miaka 21, lakini Juventus, wanataka pauni milioni 25 kumuachia mchezaji huyo. (Gazzetta dello Sport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Julai, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Julai, 2024 Reviewed by Zero Degree on 7/17/2024 08:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.