Loading...

Twiga Stars, Botswna hakuna mbabe


Timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars jana imekamilisha mechi zake za kirafiki katika ziara yake ya Tunisia kwa sare ya bila mabao dhidi ya Botswna Uwanja wa Terrain Ariana jijini Tunis.

Ikumbukwe mechi ya kwanza Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Bakari Nyundo Shime iliwachapa wenyeji, Tunisia 5-0 mabao ya Aisha Juma Mnunka matatu dakika za 14, 27 na 62, Nahodha, Opa Clement Tukumbuke dakika ya 41 na Donisia Daniel Minja dakika ya 90.

Twiga Stars imefuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) ambazo zitafanyika baadaye mwaka nchini Morocco.
Twiga Stars, Botswna hakuna mbabe Twiga Stars, Botswna hakuna mbabe Reviewed by Zero Degree on 7/14/2024 06:34:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.