Wachezaji wenye asili ya Afrika wanaong'aa Euro 2024
Mashindano ya Euro 2024 yamefikia hatua ya fainali – England itachuana na Spain. Vijana wadogo wameonyesha uwezo mkubwa, wengine wakiwa na asili ya Afrika.
Tangu mashindano yaanze, baadhi ya wachezaji wenye asili ya Afrika wanafanya vyema. Wachezaji hao wangekuwa na uwezo wa kucheza nchi fulani barani Afrika.
Hawa ni baadhi ya wachezaji wanaofanya vizuri hadi sasa kwenye michuano hiyo.
Jamal Musiala
Jamal Musiala kutoka klabu ya Bayern Munich, alizaliwa Ujerumani. Ni kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 21 tayari yuko kwenye chati ya wafungaji mabao akiwa na mabao 3. Ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Ujerumani.
Jamal Musiala
Jamala Musiala ana asili pana sana. Angeweza kuichezea England, Nigeria au Poland. Baba yake ana asili ya Nigeria na Uingereza, na Mama yake ni Mjerumani mwenye asili ya Poland.
Lamine Yamal
Lamine Yamal
Winga wa Barcelona amepata umaarufu baada ya kocha Xavi Xernandez kumpa nafasi ya kuchezea timu ya wakubwa.
Yamal amekuwa aking'ara katika klabu yake na hadi timu ya taifa akiwa na miaka 16 tu.
Katika msimu wa 2023/24 amecheza michezo 50 kwa Barcelona katika mashindano yote.
Katika michuano ya Euro, winga huyo ni mmoja wa wachezaji muhimu wa kocha wa Uhispania Luis de la Fuente.
Kijana huyo amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza mechi ya Euro pamoja na kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga katika michuano hiyo.
Yamal anafaa kuchezea Morocco au Guinea ya Ikweta, asili ya wazazi wake - lakini amechagua Uhispania kwa kuzaliwa.
Nico Williams

Nico Williams ni ndugu wa mchezaji wa Athletic Bilbao na mshambuliaji wa Black Stars, Inaki Williams ambaye aliamua kuichezea Ghana mwezi Agosti 2022.
Lakini kaka yake mdogo Nico Williams ambaye pia anastahili kuichezea Ghana, aliamua kuichezea Uhispania, kutokana na kuzaliwa huko.
Nico akitafakari safari ya wazazi wake kutoka Ghana had Uhispania anasema, “namshukuru Mungu kwamba tuko pamoja sasa na Maisha ni mazuri. Wazazi wangu wanatazama watoto wao waking’aa – kila kitu tunachofanya ni kwa ajili ya wazazi wetu.”
Katika michuano ya Euro, Nico ni mmoja wa wachezaji bora wa Uhispania.
Tetesi zimeibuka kwamba Barcelona wanataka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.
Kylian Mbappe

Baba yake Mbappe ni kutoka Cameroon na mama yake ana asili ya Algeria.
Mbappe mshambulizi wa zamani wa PSG ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani, na ana mizizi barani Afrika.
Mnamo Julai 2023, alipotembelea Yaounde, alisema: "Ni heshima kuwa pamoja na familia yangu na kuonana na marafiki wote ambao wanaonyesha upendo mwingi," Mpabbe aliwaambia wanahabari.
"Nina mipango na miradi mingi kwa ajili ya Cameroon kwa watoto na kwa siku zijazo."
Mbappe aliyejiunga na Real Madrid amefunga bao moja na ametoa pasi moja iliosababisha bao . Tayari timu yake ya Ufaransa imeomndolewa katika michunao hiyo baada ya kusakamwa 2-1 na Uhispania atika mechi ya nusu Fainali.
Kwadwo Antwi Duah

Kwadwo aliifungia Switzerland dhidi ya Hungary katika mchezo wa ufunguzi. Mshambulizi mwenye umri wa miaka 27 anachezea klabu ya Ludogoretz ya Bulgaria.
Alizaliwa London na wazazi kutoka Ghana mwaka 1997. Ni mmoja wa wachezaji watatu waliofunga kwenye mechi ya kwanza katika timu ya taifa ya Switzerland.
Baada ya mchezo huo alisema: "Huu ni mchezo wangu wa pili wa kimataifa, na nimefunga bao langu la kwanza - ninafuraha sana.”
Katika majira ya kiangazi ya 2022, alipokea mwaliko kutoka Chama cha Soka cha Ghana kucheza mechi za mchujo za kombe la dunia la 2022 dhidi ya Nigeria, lakini alikataa ofa hiyo.
Breel Embolo
Embolo anachezea Monaco, aliifungia Switzerland bao la 3 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Hungary.
Alizaliwa London na wazazi kutoka Ghana mwaka 1997. Ni mmoja wa wachezaji watatu waliofunga kwenye mechi ya kwanza katika timu ya taifa ya Switzerland.
Baada ya mchezo huo alisema: "Huu ni mchezo wangu wa pili wa kimataifa, na nimefunga bao langu la kwanza - ninafuraha sana.”
Katika majira ya kiangazi ya 2022, alipokea mwaliko kutoka Chama cha Soka cha Ghana kucheza mechi za mchujo za kombe la dunia la 2022 dhidi ya Nigeria, lakini alikataa ofa hiyo.
Breel Embolo
Familia ya Embolo ni asili ya Cemeroon. Katika kombe la Dunia la 2022, Embolo hakusherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Cameroon.
Tangu alipocheza kwa mara ya kwanza 2015, sasa amecheza mechi 60 kwa Switzerland na anatazamia kucheza zadi Euro.
Embolo mwenye umri wa miaka 27, anatembelea Cameroon kwa ajili ya likizo na pia familia na marafiki.
Manuel Obafemi Akanji
Akanji ana mama wa Switzerland na baba kutoka Nigeria. Baba yake pia alicheza mpira.
Manuel Obafemi Akanji
Akanji alisema, “Nchini Nigeria, nataka kuwasaidia watoto ambao hawajapata bahati kama niliyo nayo mimi nchini Uswizi.”
Mlinzi huyo wa Manchester city anasema Burna Boy ndiye msanii anayempenda zaidi.
Ni mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya Switzerland.
Bukayo Saka
Alizaliwa na wazazi kutoka Nigeria. Winga wa Arsenal anaiwakilisha England katika ngazi ya vijana na timu kubwa pia.
Shirikisho la Soka la Nigeria halijajaribu kumleta Saka lakini haiwezekani kufanya hivyo baada ya kucheza katika timu ya vijana nchini Uingereza.
Saka amefanya vyema ndani ya Arsenal msimu uliopita kiasi kwamba mashabiki wa England wanatumai ataibuka kuwa mfungaji bora katika michuano ya Euro.
Jeremy Frimpong
Jeremy Frimpong ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Bayer Leverkusen, iliyoshinda taji akiwa na mabao 8 msimu uliopita.
Ana umri wa miaka 23, amecheza michezo 31 katika klabu yake kabla ya kocha wa Uholanzi, Ronald Koeman kumwita kwa ajili ya Euro.
Chama cha soka cha Ghana kilimwita Frimpong lakini alikataa mwaliko wa kuichezea Ghana.
“Kocha wa Ghana alinipigia simu mwaka 2023, lakini nia yangu ni kuichezea Uholanzi,” anasema.
Tayari timu yake ya Uholanzi imeondolewa katika mashindano hayo baada ya kufungwa 2-1 na England katika mechi ya nusu fainali .
Wachezaji wenye asili ya Afrika wanaong'aa Euro 2024
Reviewed by Zero Degree
on
7/11/2024 11:43:00 AM
Rating: