Ujenzi kituo cha kupoza umeme Ifakara kuongeza fursa za uwekezaji – DC ULANGA
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Mhe. Dkt. Julius Ningu amesema kuwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ifakara, kutaongeza wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya madini.
Mhe. Dkt. Ningu amesema kuwa awali kabla ya ujenzi na kuanza kazi kwa kituo hicho umeme ulikuwa haukuwa wa uhakika kama sasa na hivyo baadhi ya wawekezaji kushindwa kufanya uwekezaji mkubwa sababu ya awali ya changamoto ya umeme.
Mkuu huyo wa Wilaya ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika sekta ya biashara, kilimo na madini na kusema kuwa milango iko wazi kuwasaidia wawekezaji.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wamewezesha ujenzi wa kituo hicho ambacho kimewezesha kuwa na umeme wa uhakika katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Ifakara.
Ujenzi kituo cha kupoza umeme Ifakara kuongeza fursa za uwekezaji – DC ULANGA
Reviewed by Zero Degree
on
12/16/2024 06:02:00 PM
Rating: