Loading...

Wataalamu Afrika Mashariki wajadili nishati safi ya kupikia jijini Afrika


Kongamano la kwanza la Nishati Safi ya Kupikia Afrika Mashariki  linaendelea jijini Arusha.


Leo tarehe 7 Mei, 2025 ambayo ni Siku ya Pili ya Kongamano, Wataalam kutoka Tanzania, Rwanda, Kenya, Burundi, Uganda na Malawi  wanaendelea na majadiliano kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo mbinu bora za utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, maarifa na kupata uzoefu jinsi kila nchi inavyotekeleza ajenda hiyo.


Majadiliano hayo pia yanaangazia masuala ya  uvumbuzi wa teknolojia za Nishati Safi ya Kupikia  na  masoko.


Katika kongamano hilo Wataalam pia wamefahamu hali ya matumizi ya  Nishati Safi ya Kupikia katika eneo la Afrika Mashariki, changamoto zilizopo, fursa  na hatua za kuchukua ili kufikia malengo yaliyowekwa katika kila nchi.








Wataalamu Afrika Mashariki wajadili nishati safi ya kupikia jijini Afrika Wataalamu Afrika Mashariki wajadili nishati safi ya kupikia jijini Afrika Reviewed by Zero Degree on 5/07/2025 01:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.