Loading...

Timu yetu imejiandaa vizuri kuikabili Burkina Faso - Kocha Hemed


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Bw. Hemed Suleiman Ali, amesema kuwa wachezaji wamejiandaa vizuri kuikabili timu ya Burkina Faso kwenye mechi ya ufunguzi itakayofanyika Agosti 02, 2025, jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo amebainisha hayo Julai 29, wakati wakiwa katika mazoezi ya kwanza baada ya kurejea kutoka katika mashindano ya CECAFA, Karatu, mkoani Arusha, ambapo ameeleza kuwa timu ipo tayari kupambana na Burkina Faso.

"Wachezaji wako tayari, kiakili na kimwili kupambana dhidi ya wapinzani wao kwenye michuano hii na tunaomba watanzania waendelee kutuunga mkono. Tutahakikisha tunapigana na kufanya vizuri kwenye mashindano haya" amesema kocha Hemed.
Timu yetu imejiandaa vizuri kuikabili Burkina Faso - Kocha Hemed Timu yetu imejiandaa vizuri kuikabili Burkina Faso - Kocha Hemed Reviewed by Zero Degree on 7/30/2025 08:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.