Mwaka huu tunapiga kichwani tu - Ally Kamwe
Kuelekea uzinduzi wa wiki ya wananchi utakaofanyika kesho katika viwanja vya Zakhiem, Yanga wanatarajia. Meneja Habari wa klabu hiyo Ally Kamwe amesema kuwa watafanya maandamano makubwa na ya kihistoria jijini Dar es Salaam.
“Uzinduzi wa kuelekea wiki ya wananchi utafanyika kesho katika viwanja vya Zakhiem, tunataka kufanya maandamano makubwa na ya kihistoria, tunataka DSM nzima iwe kijani na njano, kuanzia majira ya saa tano kila mtu afike Zakhiem Mbagala. Mwenye baiskel, mwenye daladala, mwenye pikipiki kesho ni historia ya mpira inaenda kuzinduliwa, tutatambulisha baadhi ya wasanii watakaokuwepo Siku ya Mwananchi.”
“Leo tumefanya mkutano wa kwanza kuelekea siku ya Mwananchi, lakini tayari tumeshauza tiketi zote za VIP A. Kimsingi tamasha hili limeshavuka kuwa tamasha la michezo ni Tamasha la kihistoria, kama hujanunua tiketi mpaka sasa una dalili za kupoteza fursa adhimu ya kushuhudia kilele cha wiki ya Mwananchi”
“Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa na Slogan za kupeana matumaini, tumekubaliana huu ni msimu wa vitendo na tumegundua watu bado wanataka dozi, kuanzia sasa tunaenda kupiga kichwani tu. Hiyo ndio slogan yetu, Tukipiga kichwani tunacheza na ufahamu. Mwaka huu ni kichwa tu, tumeweka kabisa nyundo kwa ajili ya wale wanaokaza fuvu” Ally Kamwe

Reviewed by Zero Degree
on
9/02/2025 12:35:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
9/02/2025 12:35:00 PM
Rating: