Loading...

Rasmi Luhaga Mpina (ACT) ameteuliwa kugombea urais wa Tanzania


Mgombea Urais kupitia Chama Cha ACT Wazalendo Luhaga Joelson Mpina leo Jumamosi ya Septemba 13, 2025 amefika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Posta, jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya kurudisha fomu yake ya kugombea Urais.

Kwa Mujibu wa Maamuzi ya Mahakama, sasa ni rasmi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Inec imemteua Luhaga Mpina Kugombea Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Kupitia Chama Cha ACT -Wazalendo, huku mgombea mwenza akiwa ni Bi. Fatma Ferej.

Uteuzi huo umefanyika asubuhi ya leo katika ofisi za INEC jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa INEC Jaji Jacobs Mwambegele amewakabidhi wagombea hao fomu ya uteuzi.

Na kama ulivyo utaratibu kwa vyama vyote, mara baada ya Mpina kuteliwa rasmi INEC wametoa gari na dereva kwa mgombea huyo lakini uongozi wa chama hicho pamoja na kushukuru kwa huduma hiyo wamesema hawachukui gari hilo kwa sasa.

Naye mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele amesema kwa kuwa wamekataa basi gari hilo litatumika katika shughuli nyingine.
Rasmi Luhaga Mpina (ACT) ameteuliwa kugombea urais wa Tanzania Rasmi Luhaga Mpina (ACT) ameteuliwa kugombea urais wa Tanzania Reviewed by Zero Degree on 9/13/2025 11:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.