TFF imeufungia uwanja wa Sokoine Mbeya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa Sokoine, Mbeya kutumika kwa michezo ya Ligi kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Hiyo ni kwa sababu miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya Leseni za Klabu.
Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama kanuni zinavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.
TFF imeufungia uwanja wa Sokoine Mbeya
Reviewed by Zero Degree
on
10/15/2025 01:02:00 PM
Rating:
