Milioni 288 zakusanywa na Polisi Morogoro ndani ya mwezi mmoja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei.
Morogoro.Polisi Morogoro imefanikiwa kuingiza Sh 288 milioni kutokana na tozo mbalimbali za makosa ya usalama wa barabarani kwa kipindi cha Mei mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema jana kuwa makosa hayo yamepatikana baada ya operesheni maalumu kufanywa na jeshi hilo kuanzia Mei Mosi hadi Mei 30.
Amesema kiasi hicho cha fedha kilipatikana kutokana na jumla ya makosa 9,612 kwa magari na pikipiki katika mkoa wa Morogoro.
Alitaja makosa ya magari kuwa ni mwendo kasi makosa 2661, ubovu wa magari makosa 988, kukiuka ratiba makosa 275, kuzidisha abiria makosa 113, kutokuwa na bima makosa 114 na mengineyo 2,908.
ZeroDegree.
Milioni 288 zakusanywa na Polisi Morogoro ndani ya mwezi mmoja.
Reviewed by Zero Degree
on
6/01/2016 07:26:00 PM
Rating: