Loading...

Walioandaa mgomo Chuo Kikuu Dar [ UDSM ] kuchukuliwa hatua kali.


Dar es Salaam. Wanafunzi walioandaa mgomo wa jana Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya Chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha Menejimenti. 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo taaluma Florens Luoga amesema kuwa hadi sasa mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinendelea na uchunguzi kubaini nani alihusika na ni kwa namna gani na baada ya hapo hatua za kinidhmu zitafuata.

“Taratibu na sheria ndogo za chuo haziruhusua mtu kuandaa mkusanyiko ambao haujaidhinishwa na menejimenti na kimsingi taratibu hizo lazima ziheshimiwe ili kuzifanya kuendelea kuwa imara hivyo tunasubiri ripoti ya walio husika endapo itaonesha kuwa wanamakosa basi watachukuliwa hatua za kinmidhamu,” amesema Luoga.




ZeroDegree.
Walioandaa mgomo Chuo Kikuu Dar [ UDSM ] kuchukuliwa hatua kali. Walioandaa mgomo  Chuo Kikuu Dar [ UDSM ] kuchukuliwa hatua kali. Reviewed by Zero Degree on 6/01/2016 07:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.