Loading...

Gari lanusurika kuzama Baharini.


Gari lenye namba za usajili T 709 AYW likiwa limeegeshwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi baada ya kutofuata sheria za vivuko, gari hilo likiwa limesheheni barafu ambapo haikufahamika mara moja ilikuwa ikipelekwa wapi. 

Inakadiriwa mnamo majira ya saa 11: 25 alfajiri, gari hilo likiingia katika kivuko cha MV Lami mapema leo hii lilinasa kwenye mlango wa kivuko hicho kwa kile kinachodaiwa ni kuzidisha mzigo mkubwa na kusababisha kunasa katika mlango huo.

Kitendo hicho kilisababisha MV Lami kusukumwa na gari hilo, ikabidi barafu iliyokuwemo ndani ya kivuko hicho kupakuliwa kisha gari hilo kuvutwa na gari lingine lenye namba za usajili T 661 AXB na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kigamboni Jijini Dar es Salaam. 




ZeroDegree.
Gari lanusurika kuzama Baharini. Gari lanusurika kuzama Baharini. Reviewed by Zero Degree on 6/01/2016 07:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.