Loading...

Muswada wa kuanzishwa kwa mahakama ya rushwa watua bungeni.


Dodoma. Serikali imewasilisha muswada bungeni wa kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya Rushwa. 

Watakaokutwa na hatia ya makosa ya rushwa au uhujumu uchumi, watafungwa kifungo kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30.

Kuanzishwa kwa mahakama hiyo ni kutimiza ilani ya CCM na ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Aliahidi kuwa ataianzisha ili kushughulika na mafisadi pamoja na wahujumu uchumi.

Kwa mujibu wa muswada huo, mahakama hiyo inaanzishwa katika marekebisho ya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 yatakayofanyika katika Kifungu cha 3.




ZeroDegree.
Muswada wa kuanzishwa kwa mahakama ya rushwa watua bungeni. Muswada wa kuanzishwa kwa mahakama ya rushwa watua bungeni. Reviewed by Zero Degree on 6/02/2016 12:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.