Loading...

Wahamiaji haramu 71 kutoka Ethiopia wakamatwa wilayani Temeke.


Dar es Salaam. Idara ya Uhamiaji wilayani Temeke mkoani hapa, inawashikilia wahamiaji haramu 71 kutoka Ethiopia kwa tuhuma za kuingia na kuishi nchini kinyume cha sheria.

Ofisa wa Uhamiaji wa Wilaya ya Temeke, George Goda alisema watu hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana wakiwa ufukweni mwa Bahari ya Hindi eneo la Kijiwe Mtu.

Watu hao walikuwa wamepakiwa kwenye lori aina ya Scania tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Afrika Kusini.

Goda alisema walipowahoji walidai kuwa walipanda boti kuja nchini wakitokea Mombasa.

Hata hivyo, alisema katika tukio hilo wanawashikilia pia dereva na kondakta wa gari hilo ambao ni wakazi wa Mkoa wa Mbeya wanaoendelea kuhojiwa.





ZeroDegree.
Wahamiaji haramu 71 kutoka Ethiopia wakamatwa wilayani Temeke. Wahamiaji haramu 71 kutoka Ethiopia wakamatwa wilayani Temeke. Reviewed by Zero Degree on 6/02/2016 01:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.