Loading...

Polisi zaidi ya 2000 watatumika kulinda amani katika mechi ya Atletico na Real Madrid

Walinzi zaidi ya 2,000 watatumiwa kudumisha usalama na kudhibiti mashabiki wakati wa mechi ya nusufainali ya mkondo wa kwanza kati ya Real Madrid na Atletico Madrid katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Mechi hiyo itakayochezewa Santiago Bernabeu siku ya Jumanne imeorodheshwa kama yenye "hatari kubwa" na usalama "utaimarishwa", maafisa wasimamizi wa jiji la Madrid walisema Ijumaa.

Uefa wameamrisha usalama katika mechi za klabu Ulaya uimarishwe baada ya shambulio kwenye basi la timu ya Borussia Dortmund mnamo 11 Aprili.

Atletico watakuwa na mashabiki 4,000 katika uwanja huo wa Real unaotoshea mashabiki 80,000.

Kawaida ni mashabiki wachache sana husafiri kuhudhuria mechi za ugenini Uhispania.

Idadi ya walinzi tarehe 2 Mei itakuwa ya juu zaidi ya waliokuwepo wakati wa mechi iliyopita ya Real Ulaya dhidi ya Bayern Munich polisi wa kukabiliana na fujo walipokabiliana na mashabiki wageni wakati wa mapumziko.

Kulikuwa pia na fujo mechi ya robofainali ya Atletico nyumbani, polisi wakikabiliana na mashabiki wa Leicester City.
Polisi zaidi ya 2000 watatumika kulinda amani katika mechi ya Atletico na Real Madrid Polisi zaidi ya 2000 watatumika kulinda amani katika mechi ya Atletico na Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 4/29/2017 01:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.