Loading...

Ronaldo adai Pepe alikuwa bora kuliko Griezmann, Euro 2016.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amesema kuwa anaamini Mreno mwenzake, Kepler Ferreira ‘Pepe’, ndiye aliyestahili kuwa mchezaji bora wa michuano ya Euro 2016 badala ya Antoine Griezmann ambaye alipewa tuzo hiyo.
Katika mashindano hayo yaliyopigwa mwaka huu, Griezmann aliifungia timu yake ya Ufaransa mabao sita katika mechi zote pamoja na kutoa pasi mbili za mabao, lakini walilikosa taji la michuano hiyo dhidi ya Ureno kwenye mchezo wa fainali.



Pepe na Ronaldo walijumuishwa kwenye kikosi bora cha mashindano hayo baada ya kunyakua taji la Euro na Ronaldo alisisitiza kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 33 alistahili kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo.

“Kwa upande wangu, Pepe alionesha kiwango bora mwaka huu na kwa kweli huu ulikuwa msimu bora kwake,” alisema.

“Bila kipingamizi, yeye alikuwa mchezaji bora zaidi Ureno na hata ndani ya klabu yetu Real Madrid alifanya makubwa mpaka tuliponyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Nilifurahi alipoteuliwa kwenye timu bora ya michuano Euro na kwa mawazo yangu Pepe alifanya mambo makubwa Euro.”

Ronaldo ni mmoja wachezaji watatu waliokuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya msimu huu, sambamba na mchezaji mwenzake wa Madrid, Gareth Bale na Griezmann, ambapo mshindi alitarajiwa kutangazwa jana Alhamisi.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Ronaldo adai Pepe alikuwa bora kuliko Griezmann, Euro 2016. Ronaldo adai Pepe alikuwa bora kuliko Griezmann,  Euro 2016. Reviewed by Zero Degree on 8/27/2016 10:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.