Loading...

Nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry apata kazi mpya timu ya taifa Ubelgiji.

Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez amesema nyota wa zamani wa klabu za Arsenal na Barcelona, Thierry Henry, ambaye pia aling'aa sana akichezea timu ya taifa ya Ufaransa, atakuwa mmoja wa wasaidizi wake.
Henry alikuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya vijana Arsenal lakini akajiuzulu Julai baada ya meneja Arsene Wenger kumwambia kwamba hawezi kufanya kazi hiyo akiwa bado anaendelea kuwa mchambuzi wa soka kwenye runinga.

Nyota huyo huchambua soka katika Sky Sports na pia alifanya kazi na BBC Sport wakati wa Euro 2016.

Thierry Henry alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani.


Credits: BBC Swahili
ZeroDegree.
Nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry apata kazi mpya timu ya taifa Ubelgiji. Nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry apata kazi mpya timu ya taifa Ubelgiji. Reviewed by Zero Degree on 8/27/2016 10:37:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.