Kituo cha polisi chajengwa kwenye hifadhi ya Barabara.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), Luhaga Mpina.
Dodoma. Jengo la Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kipolisi ya Kimara mkoani Dar es Salaam, limejengwa kwenye hifadhi ya barabara, Bunge liliambiwa jana.
Akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), Luhaga Mpina, aliyesema jengo hilo licha ya kutumiwa na polisi, lakini liko kwenye hifadhi ya Barabara ya Morogoro.
Mnyika alitaka kujua ni lini na wapi kituo kipya cha polisi katika wilaya hiyo ya kipolisi kitajengwa.
Naibu waziri huyo alisema Serikali itajenga kituo kipya eneo la Luguluni muda wowote kuanzia sasa.
Alisema Wilaya ya Kipolisi ya Kimara ilianzishwa kufuatia kuundwa kwa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam chini ya mpango wa maboresho ya Jeshi la Polisi ya mwaka 2006 kwa lengo la kuongeza ufanisi na kusogeza huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi.
Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Kituo cha polisi chajengwa kwenye hifadhi ya Barabara.
Reviewed by Zero Degree
on
6/02/2016 01:09:00 PM
Rating: