Baraza la madiwani lakumbwa na kashfa ya Rushwa.
Kahama. Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, limekumbwa na kashfa baada ya wananchi kulituhumu kwa rushwa.
Wakazi hao wa kata 10 kati ya 18 zinazounda Halmashauri hiyo, wameiomba ofisi ya Rais (Tamisemi) kulivunja.
Wanadia kuwa rushwa imeshamiri hasa katika mgogoro wa ujenzi wa makao makuu yaliyoidhinishwa na Serikali yajengwe eneo la Busangi.
Wakitoa malalamiko yao mbele ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, John Mongella, walisema makao hayo yaliyojengwa katika Kata ya Ntobo hayakuwa makubaliano na kwamba, yalitakiwa kujengwa Kata ya Busangi.
Walimtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) kulivunja kwa madai limejaa rushwa iliyokwamisha ujenzi wa makao hayo katika eneo walilokubaliana awali.
Mgogoro wa kupinga ujenzi huo ulianza tangu mwaka 2012 na hakukuwa na msimamo maalumu wa kata husika itakayojengwa makao hayo na mara ya mwisho walikubaliana yajengwe Kata ya Ntobo.
Baraza la madiwani lakumbwa na kashfa ya Rushwa.
Reviewed by Zero Degree
on
6/02/2016 01:17:00 PM
Rating: