Loading...

Neymar atokwa na machozi akimzungumzia Messi


Neymar alionekana akitokwa na machozi wakati alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Lionel Messi alipokuwa Barcelona.

Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain ambaye amefunga magoli 68 katika michezo 123 vigogo hao wa Hispania kwa misimu minne alionekana kuwa na hisia kali wakati akimzungumzia aliyekuwa mchezaji mwenzake.

Mbazil huyo alisema, “Kusema kweli, ni ngumu sana kwa mimi kumzungumzia Messi, kwa sababu ili kuwa ni nafasi ya pekee sana kwangu mimi katika klabu ya Barcelona, huwa nasema hivi kwa kila mtu.”




“Wakati nilipohitaji msaada zaidi, mchezaji bora duniani alikukuwepo kufanya hivyo. Alisema, ‘njoo, niko hapa kukusaidia.’”

Kwa mujibu wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27, Messi ndiye alimpa hamasa ya kuonyesha uwezo wake binafsi baada ya uhamisho wake kwenda Camp Nou. Mshindi huyo wa tuzo ya Balon d’Or mara tano alimwambia Neymar asimwogope yeye wala 'mtu mwingingine yeyote klabuni’.

Ilikuwa wazi kwamba Messi alikuwa anatengeneza mazingira ya kumrithisha mikoba yake katika klabu ya Barcelona. Hata baada ya uhamisho wake uliovunja rekodi kwenda PSG, Mwajentina huyo yuko tayarri kumkaribisha kwa mikono miwili.

Kuna wakati, Messi alisema, “Nafikiri nivigumu sana kufikiri ni jinsi gani Neymar ataondoka PSG. Tungefurahi kumuona akirejea, kama mchezaji na kwa faida ya ari ya wachezaji kwenye chumba cha kubadilishia nguo.”

“Ni rafiki yangu mkubwa. Tulikuwa na wakati mzuri pamoja na wengine si kwa sana. Lakini PSG hawawezi kumruhusu Neymar aondoke kirahisi.”
Neymar atokwa na machozi akimzungumzia Messi Neymar atokwa na machozi akimzungumzia Messi Reviewed by Zero Degree on 2/26/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.