Loading...

Mazito yabainika baada ya mauaji Tanga.


Dar/Mikoani. Wakati mauaji ya watu wanane waliochinjwa usiku wa kuamkia juzi mkoani Tanga yakizua maswali lukuki na kuzidisha hofu, imebainika kuwa wauaji waliwachinja wote kuanzia sehemu ya chini ya kisogo.

Watu hao waliuawa kwa kuchinjwa katika kitongoji cha Mabatini, Kata ya Mzimama, Tanga.

Tukio hilo lilifanywa nje ya nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho, ikiwa ni mwendelezo wa mauaji ya uchinjaji yaliyoikumba nchi tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Mauaji hayo yametokea wakati mkoa wa Tanga ukizidi kukumbwa na matukio yanayohisiwa kuwa ni ya kigaidi tangu polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walipopambana na watu wasiojulikana kwenye mapango ya Amboni Januari 26 mwaka jana.

Source: Mwananchi




ZeroDegree
Mazito yabainika baada ya mauaji Tanga. Mazito yabainika baada ya mauaji Tanga. Reviewed by Zero Degree on 6/02/2016 01:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.