Loading...

Vivutio vya asili vya utalii China vyafungwa kuhofia Korea Kaskazini

Milima ya Changbaishan
China imetangaza kufunga vivutio vyake vya asili vya utalii kwa kuhofia madhara makubwa yatakayotokea ikiwemo maporomoko ya ardhi na milipuko ya Volcano kutokana na majaribio ya silaha za nyuklia yanayotekelezwa na Korea Kaskazini.

Maeneo ambayo serikali ya China imeshatangaza kuyafunga kwa matumizi ya umma ni kreta ya Changbaishan, Mlima Paekto ambao una volcano hai na upo mpakani kati ya Korea Kaskazini na China.

“Kutokana na usalama wa watalii na kuepusha usumbufu kwao serikali imelazimika kufunga kwa muda vituo vyetu vya utalii vya asili vilivyopo kusini mwa milima ya Changbai“,Imeeleza taarifa rasmi iliyotolewa jana na Serikali kupitia Bodi ya utalii nchini humo.

Kwa upande mwingine rais wa Marekani, Donald Trump ameguswa na vitisho hivyo na kusema kuwa tayari ameshawasiliana na Rais wa Korea Kusini na kujadiliana jinsi ya kuidhibiti Korea Kaskazini kwa kila namna juu ya utengenezaji wa silaha za kinyuklia.
Vivutio vya asili vya utalii China vyafungwa kuhofia Korea Kaskazini Vivutio vya asili vya utalii China vyafungwa kuhofia Korea Kaskazini Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.