Loading...

Ajali yaua watanzania 13 nchini Uganda


WATANZANIA 13 wamefariki na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la biashara Lubanda takribani kilomita 80 kufika Kituo cha Polisi cha Fika Salama karibu na Mto Katonga Wilaya ya Mpigi, Kampala, Uganda.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya fuso yenye namba za usajili UAH 970P na coaster yenye namba T540 DLC waliokuwa wakitumia Watanzania hao wakiwemo ambao inasemekana walikuwa wakitoka kwenye harusi ya binti wa Dkt. Annette Ibingira ambaye ni mke wa mhazini wa shule ya Wazazi ya Kampala nchini Uganda Dkt. Ibingira.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Nkozi na Double Cure Clinic zilizopo nchini Uganda huku miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo imepelekwa katika Hospitali ya Gombe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Ajali yaua watanzania 13 nchini Uganda Ajali yaua watanzania 13 nchini Uganda Reviewed by Zero Degree on 9/18/2017 04:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.