Askofu aendesha maombi maalumu ya kuombea mvua nchini
Askofu wa Kanisa la Habari Njema kwa Wote la Jijijni Dar es Salaa, Charles Gadi pamoja na wasaidizi wake, wameendesha maombi maalum ya kuliombea Taifa mvua, ili ziweze kusaidia wananchi na viumbe vyote vinavyotegemea maji kupitia Baraka za mvua sehemu mbalimbali.
Tukio hilo limefanyika mapema leo Septemba 18,2017, Jijini Dar es Salaam, Askofu Gadi aliambatana na wasaidizi wake na kuliombea Taifa mvua huku akiwataka wananchi nao kuungana katika maombi hayo kwani ardhi ikiendelea kuwa kame viumbe vitapoteza maisha na hata kusababisha majanga katika nchi.
Askofu Gadi aliongeza kuwa, viongozi wengine wa dini kwa pamoja nao wanayo nafasi ya kuliombea Taifa katika hilo ili ukame usitokee. Ukame ni jambo baya na kwa uchumi, ni baya kwa afya na watu na tena ni baya viumbe hai wote wakiwemo wanyama na mimea.
Vifungu vingine ni pamoja na : Mathayo 5:45, Matendo ya Mitume 15:17 na kitabu cha Yakobo 5:17-18.
Katika hitimisho hilo, Askofu Gadi ameweka wazi kuwa, kwa maandiko hayo ya Biblia, yanaonyesha wazi kwaba mvua ni mali ya Mungu, na ameahidi pasipo shaka kwamba tukimuombaanatupatia.
“ Hivi karibuni Mamlaka ya hali ya hewa wametoa tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea upungufu mkubwa wa mvua za vulikwenye mikoa mingi hapa nchini. Sisi kama viongozi wa dini tunakubaliana na utabiri huo wa Kisayansi na ambao mara nyingi ufanikiwa, lakini haitakuwa sawa kusubiri hadi ukame utokee wakati Mungu ametupa imani na mamlaka ya kuombea dhidi ya majanga kama hayo.
Sisi kama Goods News for All, kwa kushirikiana na dini na madhehebu mbalimbali tumekuwa tukiendesha mikutano ya kuomba dhidi ya ukame tangu mwaka 2006, ambapo ni zaidi ya miaka 11 sasa” alieleza Askofu Gadi.
Askofu Gadi aliongeza kuwa, viongozi wengine wa dini kwa pamoja nao wanayo nafasi ya kuliombea Taifa katika hilo ili ukame usitokee. Ukame ni jambo baya na kwa uchumi, ni baya kwa afya na watu na tena ni baya viumbe hai wote wakiwemo wanyama na mimea.
Aidha, Askofu Gadi alinukuu baadhi ya vifungu vya Biblia ikiwemo: Kumbu kumbu 28:12 “Atakufunulia bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; Nawe utakopesha mataifamengi,wala hutakopa wewe."
Vifungu vingine ni pamoja na : Mathayo 5:45, Matendo ya Mitume 15:17 na kitabu cha Yakobo 5:17-18.
Katika hitimisho hilo, Askofu Gadi ameweka wazi kuwa, kwa maandiko hayo ya Biblia, yanaonyesha wazi kwaba mvua ni mali ya Mungu, na ameahidi pasipo shaka kwamba tukimuombaanatupatia.
Askofu aendesha maombi maalumu ya kuombea mvua nchini
Reviewed by Zero Degree
on
9/18/2017 04:28:00 PM
Rating: