Loading...

PSG kusajili watatu kutoka Uhispania kwenye majira ya joto

Isco
Paris Saint-Germain ni moja kati ya klabu kubwa barani Ulaya na inapigania kufika katika kilele cha mafanikio. Mara nyingi huwa wanatafuta wachezaji wazuri na kuwasajili. Katika kipindi cha majira ya joto kilichopita, klabu hiyo ilimsajili Neymar kutoka Barcelona na kuvunja rekodi ya ada kubwa ya usajili na pia walimsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco.

Wengi waliamini klabu hiyo itakamilisha lengo lake la kushinda taji la Ligi ya Mabingwa. Lakini walishindwa baada ya kutolewa nje ya michuano hiyo kwenye hatua ya 16 bora.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, klabu hiyo inapanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha tena kwenye majira ya joto. PSG wanataka kumsajili golikipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak, kiungo wa Real Madrid, Isco na beki wa Barcelona, Samuel Umtiti, na pia wanataka kumteua Diego Simeone kuwa meneja wao mpya, kwa mujibu wa taarifa ya Don Balon .

PSG wako tayari kutumia zaidi ya pauni milioni 250 kwa ajili ya uhamisho wa wachezaji watatu. Wachezaji hao wanahusishwa na kuondoka katika klabu zao kwenye majira ya joto. Isco hafurahii kukosa nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid, Umtiti anataka ongezeko kubwa kwenye mshahara wake anaolipwa na Barcelona bado haijakubaliana na ombi lake na Oblak amekuwa akihusishwa na kuondoka Atletico kwa muda mrefu.

Uwezekano wa Unai Emery kuondoka kwenye majira ya joto ni mkubwa sana na PSG wanata meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone achukue nafasi yake.
PSG kusajili watatu kutoka Uhispania kwenye majira ya joto PSG kusajili watatu kutoka Uhispania kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 4/02/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.