Loading...

NAFASI za wabunge wa UPINZANI Bungeni zavamiwa na wabunge wa CCM.


KUSUSA na kutolewa nje mara kwa mara kwa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, kumegeuka kivutio baada ya baadhi ya wabunge wa CCM kujaza nafasi zinazokuwa wazi za upinzani, wakati wakiwa wamesusa.

Mbali na kujaza nafasi hizo na kuchangia hoja huku wakijiita wabunge wa kambi mbadala, baadhi ya wabunge hao wa CCM jana waliamua kuchukua jukumu la maswali ya wabunge wa upinzani, wakati wabunge hao wanapokuwa nje katika harakati zao za kususa au baada ya kutolewa nje.

Juzi usiku wakati Bunge lilipokaa kuwa Kamati ya Matumizi ya kupitisha Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (CCM) maarufu Profesa Majimarefu na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto (CCM), walikalia viti vya viongozi wa upinzani na kujitambulisha kuwa kambi mbadala.

Akichangia hoja ya kuendeleza miradi ya maji iliyosimama, Mwamoto alisema; “Upande wetu wa kambi mbadala, tunatoa ushauri kwa CCM, kuwekeza katika uvunaji wa maji kwani mwaka huu mvua zimenyesha na maji mengi tumeyapoteza.”

Naye Ngonyani akichangia hoja hiyo alisema; “natoa ushauri kwa CCM, sisi kambi mbadala tunashauri mabwawa ya maji yaliyochimbwa, yaondolewe magugu maji kwa kuwa serikali ilitumia fedha nyingi kuyachimba, lakini magugu hayo yanayakausha.”





ZeroDegree.
NAFASI za wabunge wa UPINZANI Bungeni zavamiwa na wabunge wa CCM. NAFASI za wabunge wa UPINZANI Bungeni zavamiwa na wabunge wa CCM. Reviewed by Zero Degree on 6/01/2016 07:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.