Loading...

Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde agoma kusoma hotuba ya upinzani.


David Silinde akiondoka bungeni baada ya kukataa kusoma bungeni maoni ya kambi hiyo kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17, mjini Dodoma leo. 

Dodoma. Msemaji wa Kambi ya upinzani kwa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde amegoma kusoma hotuba ya kambi hiyo bungeni kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa Naibu Spika, Tulia Ackson katika kuliendesha Bunge.

Baada ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwasilishwa taarifa yake, Dk Tulia alimtaka msemaji wa upinzani kuwasilisha taarifa yake, bila wabunge wengine wa upinzani kuwamo ndani ya Bunge kumpinga naibu spika.

Baada ya kuitwa, Silinde alitokea nje moja kwa moja na kusema kuwa anaomba hotuba ya Kambi hiyo iingie kwenye kumbukumbu za Bunge kama ilivyo ila hataisoma kutokana na kutoridhishwa na Naibu Spika, kisha akatoka nje.




ZeroDegree.
Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde agoma kusoma hotuba ya upinzani. Naibu Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde agoma kusoma hotuba ya upinzani. Reviewed by Zero Degree on 6/01/2016 07:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.