Loading...

Luis Suarez afikia Rekodi ya Crespo.


Rekodi zilikuwa zimesinyaa kwa muda mchache lakini Cristiano Ronaldo ameziamsha baada ya kufunga magoli mengi timu yake ya taifa ya Ureno ndipo rekodi nyingine zinafuatia, sasa upande wa pili umegeuka na rekodi zake kupitia timu ya taifa.

Mfungaji bora wa La Liga na klabu ya Barcelona amemfikia mchezaji wa zamani wa Chelsea Hernan Crespo kwa rekodi ya ufungaji bora kwa timu za mataifa ya bara la Amerika kusini, kumbuka Crespo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina .


Rekodi aliyoifikia Suarez ni ile ya kufunga magoli 19 katika hatua ya makundi kwa maana ya ‘Qualification stage’ kwa bara la Amerika Kusini ambapo Crespo alikuwa anaongoza kwa bara hilo kabla ya nyota huyo kumfikia kwa goli lake gumu alilolifunga na kupata sare ya 2-2 dhidi ya Colombia.

ZeroDegree.
Luis Suarez afikia Rekodi ya Crespo. Luis Suarez afikia Rekodi ya Crespo. Reviewed by Zero Degree on 10/13/2016 09:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.