Loading...

Simba na Yanga watoka kifua mbele, ..Stand United waikalisha Azam Fc.

Wachezaji wa wekundu wa Msimbazi Simba.

Wekundu wa msimbazi Simba Wakicheza ugenini katika dimba la Sokoine waliibuka na ushindi mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City.


Timu ya wanainchi Dar young Africans nao wakachomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wakatamiwa na Mtibwa Sugar.

Mwadui Fc wakawachapa African Lyon kwa mabao 2-0. Chama la wana Stand United wamewachapa wanalamba lamba Azam FC bao 1-0.

Jkt Ruvu na Tanzania Prisons wametosha nguvu kwa sare ya bila kufungana. Nao Mbao Fc waliwachapa ndugu zao Toto Africans kwa mabao 3-1

Majimaji wamelala nyumbani kwa kuchapwa bao 1-0 na kagera Sugar. Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa Kwa Ruvu Shooting kuwa wenyeji wa Ndanda.


ZeroDegree.
Simba na Yanga watoka kifua mbele, ..Stand United waikalisha Azam Fc. Simba na Yanga watoka kifua mbele, ..Stand United waikalisha Azam Fc. Reviewed by Zero Degree on 10/13/2016 09:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.