Loading...

TANZIA: Aliyekuwa meya wa jiji la Dar, Dkt. Didas Masaburi afariki dunia.

Usiku wa saa tatu, Oktoba 12.2016 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na familia kwa ujumla wamepokea kwa masikitiko kuhusu kifo cha Kada wa Muda mrefu wa Chama hicho, Dkt Didas Masaburi.

Masaburi amekuwa kada mtiifu ndani ya chama chake alikuwa mtu mahiri kwenye uchaguzi wa ndani ya chama kuliko hata sekta nyingine ni dhahiri kuwa alikifia chama.

Amewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es salaam sambamba na kuwa Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki.

Dkt Masaburi ni miongoni mwa viongozi wa CCM walioivishwa ukada kutokea Umoja wa Vijana UVCCM enzi hizo akiwa makini kabisa yeye, marehemu Rashid Mchatta na William Vangimembe Lukuvi.

Kifo chake kimejiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa anapatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Taarifa za awali zimebaini kuwa msiba upo nyumbani kwake Segerea Jijini Dar es salaam.

Innaillilah Wainna Illilah Rajiun, Sote ni wa Mwenyezi na kwake tutarejea.


ZeroDegree.
TANZIA: Aliyekuwa meya wa jiji la Dar, Dkt. Didas Masaburi afariki dunia. TANZIA: Aliyekuwa meya wa jiji la Dar, Dkt. Didas Masaburi afariki dunia. Reviewed by Zero Degree on 10/13/2016 09:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.