Loading...

Emmanuel Okwi aanza kusababisha mambo Uganda

KAMA ulidhani mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi, ameshuka kiwango ndiyo maana akatemwa huko Denmark, utakuwa umekosea kwani mkali huyo wa mabao ameshaanza kutupia nchini kwao Uganda.

Okwi ambaye alivunja mkataba wake na kikosi cha SonderjyskE ya nchini Denmark baada ya kuchoshwa na benchi, amejiunga na timu yake ya zamani ya SC Villa na mwishoni mwa wiki aliiokoa na kipigo baada ya kufunga bao dhidi ya Jinja Municipal Hippos mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu nchini Uganda, Okwi aliifungia timu yake hiyo ya Villa bao dakika ya 30, huku kikosi chake hicho kikimaliza pungufu baada ya mlinzi Henry Katongole kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.

Kwa upande wao JMC Hippos, walisawazisha bao katika dakika ya 52 kupitia kwa Jimmy Jalendo, ambapo mpaka mpambano huo unamalizika, timu hizo zililazimika kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Huo ni mchezo wa pili kwa Okwi kuichezea timu hiyo tangu kujiunga nayo, kwani alianza Jumanne iliyopita dhidi ya Bright Stars mchezo uliomalizika kwa suluhu ya 0-0 ambapo michezo yote hiyo straika huyo alicheza vizuri.
Emmanuel Okwi aanza kusababisha mambo Uganda Emmanuel Okwi aanza kusababisha mambo Uganda Reviewed by Zero Degree on 2/14/2017 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.