Loading...

Msanii mkongwe nchini, Khalid Mohamed [TID] amekili kutumia dawa za kulevya

MSANII wa bongofleva, Khalid Mohamed 'TID' jana alikiri kwenye mkutano uliokuwa umeandaliwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza katika mkutano huo, TID alikiri kuwa miongoni mwa wasanii wa muziki huo wanatumia madawa ya kulevya.

‘’Kweli nimekuwa miongoni mwa wasanii wanao tumia madawa ya kulevya na nimeikosea sana familia yangu na nimewakosea sana mashabiki wangu hivyo nakiri kuwa sitojiingiza tena katika matatizo haya na nitakuwa mstari wa mbele kupambana na vita hivi, kwa sasa mimi situmii tena’’, alisema TID

Aidha,TID alimpongeza Rais wa Tanzania, John Magufuli na Makonda kwa kuanzisha oparesheni juu ya madawa ya kulevya ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa sana kuwahamasisha vijana wengi kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.

TID mara kwa mara alikuwa akihusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya na alikuwa akikataa kujihusisha nayo mpaka alipotajwa na Makonda kwenye 'kamata kamata' ya watumiaji na wauzaji wa madawa hayo.

Wasanii wengine walihusishwa na madawa hayo ni pamoja na Wema Sepetu, Petitman, Recho, Mr blue, Babuu wa Kitaa pamoja na Dogo Hamidu.
Msanii mkongwe nchini, Khalid Mohamed [TID] amekili kutumia dawa za kulevya Msanii mkongwe nchini, Khalid Mohamed [TID] amekili kutumia dawa za kulevya Reviewed by Zero Degree on 2/14/2017 12:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.