Loading...

Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho 'FA' iko hapa, ..Simba kucheza na African Lyon

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) jana limetoa ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho raundi ya sita ambapo Simba imepangwa kucheza na African Lyon huku Yanga ikiumana na timu ya daraja la kwanza ya Kiluvya.

Katika ratiba hiyo iliyotolewa jana, Azam yenyewe imepangiwa kucheza na Mtibwa Sugar huku Mbeya City wakiumana na ndugu zao, Tanzania Prisons.

Ratiba hiyo inaonyesha Simba watacheza mchezo wao Machi Mosi kwenye Uwanja wa Taifa wakati Yanga watacheza na Kiluvya siku sita baadae.

Azam yenyewe itacheza mchezo wake na Mtibwa Februari 24 kwenye Uwanja wa Azam Complex. Ratiba hiyo inaonyesha pia siku hiyo, Kagera Sugar itacheza na Stand United kwenye Uwanja wa Kaitaba wakati Madini itaikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Amri Abeid jijini Arusha.

Toto African imepangwa kucheza na ‘ndugu’ zao Mbao FC na mchezo wao utachezwa Februari 26 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Might Elephant iliyoing’oa Majimaji kwenye hatua ya raundi ya tano, yenyewe imepangiwa kucheza na Ndanda FC na mchezo huo utachezwa Februari 24 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho 'FA' iko hapa, ..Simba kucheza na African Lyon Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho 'FA' iko hapa, ..Simba kucheza na African Lyon Reviewed by Zero Degree on 2/07/2017 12:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.