Loading...

Mwanafunzi wa sekondari akamatwa na kete 24 za cocaine Jijini Mbeya

Vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda imetua jijini Mbeya baada ya polisi kutangaza kumkamata mwanafunzi anayesoma sekondari akiwa na kete 24 za cocaine eneo la Mbalizi.

Kamanda wa polisi mkoa, Dhahir Kidavashari amesema leo kuwa polisi wamemkamata mwanafunzi huyo akiwa anaziuza dawa hizo kwa watu mbalimbali na kwamba upelelezi wa kuwadaka mapapa unaendelea.

Kukamatwa kwa kijana huyo kunatokea siku moja baada ya Rais John Magufuli kuunga mkono kazi ya Makonda huku akiwaagiza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wote wanaojihusisha na dawa za kulevya bila kujali huyu ni nani.

Kidavashari amesema kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya ilikuwa ikiendelea, lakini sasa imepata msukumo mpya ambao unalenga kuukata mnyororo mzima wa mtandao unasambaza dawa hizo.
Mwanafunzi wa sekondari akamatwa na kete 24 za cocaine Jijini Mbeya Mwanafunzi wa sekondari akamatwa na kete 24 za cocaine Jijini Mbeya Reviewed by Zero Degree on 2/07/2017 07:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.