Loading...

Alichosema mshauri wa Antonie Griezmann endapo nyota huyo atasajiliwa na Man U

Mshauri wa mwonekano wa staa wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann ameshauri kuwa endapo dili la uhamisho la mchezaji huyo kujiunga Manchester United litakamilika basi ni vyema akapewa jezi namba 7 ambayo ni jezi yenye heshima kubwa klabuni hapo.

Mshauri huyo, Sebastien Bellencontre alisema uhamisho huo ni wa kibiashara zaidi na ili ufanikiwe litakuwa ni jambo jema endapo atapewa jezi ambayo imetumiwa na wachezaji wenye heshima kubwa Man United na hiyo inaweza kuwa njia nzuri ya kutumia uwepo wake kufanya biashara.

“Niliposoma habari kuhusu uhamisho wa kwenda Manchester United nilifikiri kuwa huo utakuwa ni uhamisho wa kibiashara, atacheza timu ya zamani ya Beckman ambaye ni mtu anayemtizama katika uchezaji wake,

“Namba ile ile iliyokuwa ikitumiwa na mkongwe huyo ndiyo anatakiwa kuitumia, na hilo ndilo linalofanyika katika michezo,” alisema Bellencontre.
Alichosema mshauri wa Antonie Griezmann endapo nyota huyo atasajiliwa na Man U Alichosema mshauri wa Antonie Griezmann endapo nyota huyo atasajiliwa na Man U Reviewed by Zero Degree on 2/07/2017 12:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.