Loading...

Mkutano wa Nape wazuiwa Protea, ...azungumza na wanahabari chini ya ulinzi wa polisi

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye 

Taarifa hizo ambazo hata hivyo hazijathibitishwa zimeeleza kuwa Kamanda wa Polisi wa Kinondoni Suzana Kaganda amepiga simu hotelini na kuzuia mkutano huo.

Hata hivyo baadhi ya waandishi waliokuwapo eneo hilo walizungumza na Nape kwenye simu ambaye aliwaahidi kuwa atafika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na kuzungumza nao.

Azungumza chini ya ulinzi wa polisi:

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amezungumza na wanahabari nje ya hoteli ya Protea baada ya mkutano wake kuzuiwa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni.
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amezungumza na wanahabari nje ya hoteli ya Protea baada ya mkutano wake kuzuiwa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni.

Katika mkutano huo, Nape alionyeshwa kushangazwa na kitendo cha polisi kumnyooshea bunduki alipokuwa akitaka kuzungumza na wanahabari katika eneo hilo.

“Mimi ni mtu mdogo sana ndani ya Tanzania, Nape hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania,” alisema Nape

Nape alisema hana kinyongo na uamuzi wa Rais John Magufuli kumtoa katika nafasi hiyo na amewaomba wanahabari kumpa ushirikiano Waziri mpya, Harrison Mwakyembe.

Nape ameondoka katika eneo hilo baada ya gari lake kuzuiwa na polisi na amewaambia waandishi wa habari kuwa atawajulisha lolote litakalotokea.



Source: Mwananchi
Mkutano wa Nape wazuiwa Protea, ...azungumza na wanahabari chini ya ulinzi wa polisi Mkutano wa Nape wazuiwa Protea, ...azungumza na wanahabari chini ya ulinzi wa polisi Reviewed by Zero Degree on 3/23/2017 05:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.