Loading...

Rais Magufuli afanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri, ....Nape 'Out', Mwakiembe kujaza nafasi yake

Rais wa Tanzania, Dk. John magufuli amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harisson Mwakyembe amechukua nafasi ya Nape Nnauye na kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk Harrison Mwakyembe ambaye anakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyokuwa ikishikiliwa na Nape Nnauye.

Taarifa iliyotolewa leo asubuhi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja na wateule wote wataapishwa kesho mchana.
Rais Magufuli afanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri, ....Nape 'Out', Mwakiembe kujaza nafasi yake Rais Magufuli afanya mabadiliko kwenye baraza la mawaziri, ....Nape 'Out', Mwakiembe kujaza nafasi yake Reviewed by Zero Degree on 3/23/2017 10:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.