Loading...

Haya hapa matokeo ya mechi za kimataifa, Ujerumani yailaza Uingereza kwa ushindi wa goli 1-0

Podolski akirushwa juu na wenzake baada ya mchezo kumalizika ikiwa ni sehemu ya kumuaga nyota huyo mwenye miaka 31
Timu ya taifa ya England imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.

Bao pekee la ushindi katika mchezo huo liliwekwa kambani na mshambuliaji Lukas Podolski katika dakika ya 69 ya mchezo kwa shuti kali la umbali wa mita 25 lilomshinda kipa wa England Joe Hart.

Mchezo huu wa kirafiki ulikua ni mchezo wa mwisho kwa mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Ujerumani Lukas Podolski anayestaafu soka la kimataifa akiwa na umri wamiaka 31.


Lukas Podolski akishangilia goli alilofunga
Mshambulia huyu alianza kuichezea timu ya taifa ya wakubwa mwaka 2004 na kufunga jumla ya magoli 49 katika michezo 130.Baadhi ya timu za taifa za mchezo wa soka zimecheza michezo ya kirafiki ya kimataifa usiku wa kuamkia leo.



Scotland wakiwa nyumbani kwao wameambulia sare ya 1-1 na Canada ,Jamuhuri ya Czech imewatambia nyumbani Lithuania kwa kuwachapa mabao 3-0.

Cyprus wao wakautumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 - dhidi ya Kazakhstan, Cambodia wao wakalala nyumbani kwa kichapo cha mabao 3-2 toka kwa timu ya taifa ya India.

Djbouti wao wakawalaza Sudani ya kusini kwa maba 2-0, Yemeni wakafungwa katika uwanja wao wa nyumbani na Palestina kwa bao 1-0.

Matokeo ya Michezo Mingine ya kimataifa iliyochezwa jana:

Haya hapa matokeo ya mechi za kimataifa, Ujerumani yailaza Uingereza kwa ushindi wa goli 1-0 Haya hapa matokeo ya mechi za kimataifa, Ujerumani yailaza Uingereza kwa ushindi wa goli 1-0 Reviewed by Zero Degree on 3/23/2017 10:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.