Loading...

Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais IKULU, Gerson Msigwa athibitisha Rais kumteua Dk. Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape Nnauye

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULU, Gerson Msigwa amethibitisha Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Mabadiliko ambayo yamefanywa ni Dk. Harrison Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Prof. Palamagamba Kabudi akichukua nafasi ya Dk. Mwakyembe na kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Msigwa amesema Dk. Mwakyembe na Prof. Kabudi wataapishwa kesho mchana Ikulu, Dar.
Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais IKULU, Gerson Msigwa athibitisha Rais kumteua Dk. Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape Nnauye Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais IKULU, Gerson Msigwa athibitisha Rais kumteua Dk. Mwakyembe kuchukua nafasi ya Nape Nnauye Reviewed by Zero Degree on 3/23/2017 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.