Loading...

Evans Aveva, Kaburu wapandishwa kizimbani tena, ..kesi yao yaahirishwa hadi Agosti 22


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Agosti 7, 2017 imeahirisha kwa mara nyingine kesi ya kutakatisha fedha na kughushi nyaraka inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu hadi Agosti 22, 2017 baada ya upelelezi kutokamilika.

Wakiingia kwenye chumba cha mahakama
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mwambapa baada ya Wakili wa TAKUKURU, Kishenyi Mutalemwa kueleza kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba iahirishwe hadi tarehe nyingine, ambapo watuhumiwa wamerudishwa gerezani.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.
Evans Aveva, Kaburu wapandishwa kizimbani tena, ..kesi yao yaahirishwa hadi Agosti 22 Evans Aveva, Kaburu wapandishwa kizimbani tena, ..kesi yao yaahirishwa hadi Agosti 22 Reviewed by Zero Degree on 8/07/2017 01:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.